Siasa gani hii?
Jicho limefumba
Shavu limevimba
Mguu unachechemea
Michubuko mwili uzima
Kulikoni ndugu rafiki?
Aah! Utelezi
Jana usiku gizani
Maji yalichuruzika sakafuni
Nikateleza nikaangukia kisiki!
Siasa gani hii?
Jicho limefumba
Shavu limevimba
Mguu unachechemea
Michubuko mwili uzima!
Ah! Kisiki ndani ya nyumba?
Uongo mwingine ...
Nyuma ya paziajembamba
Ningesemaje?
Juzi nilipobururwa hadharani
Hamkuingilia!
Ni ugonvi wao wa ndani
Niliwasikia wengine mkisema
Nilijiona dhalili!
Mlipoishika midomo yenu
Ndani ya viganja vyenu
Mkinicheka ...
Leo mwanitaka niseme nini?
Wacha nivumilie vitendo vyake
Niifunike aibu yenu na yangu
Ndani ya ukimya huu
Pamoja na uongo huu Tunaouishi!
Hizi ndizo mila zetu
Na utamaduni wetu
Na maadili yetu
Lakini niambie ndugu rafiki ....
Mila na utamaduni wa nani?
Na hayo maadili?
Yanamlinda nani?
Siasa gani hii ...
Inayoyatenganisha Mambo
ya ndani na ya nje Ipate
kuhalalisha ukatili!
By Demere Kitunga
Jicho limefumba
Shavu limevimba
Mguu unachechemea
Michubuko mwili uzima
Kulikoni ndugu rafiki?
Aah! Utelezi
Jana usiku gizani
Maji yalichuruzika sakafuni
Nikateleza nikaangukia kisiki!
Siasa gani hii?
Jicho limefumba
Shavu limevimba
Mguu unachechemea
Michubuko mwili uzima!
Ah! Kisiki ndani ya nyumba?
Uongo mwingine ...
Nyuma ya paziajembamba
Ningesemaje?
Juzi nilipobururwa hadharani
Hamkuingilia!
Ni ugonvi wao wa ndani
Niliwasikia wengine mkisema
Nilijiona dhalili!
Mlipoishika midomo yenu
Ndani ya viganja vyenu
Mkinicheka ...
Leo mwanitaka niseme nini?
Wacha nivumilie vitendo vyake
Niifunike aibu yenu na yangu
Ndani ya ukimya huu
Pamoja na uongo huu Tunaouishi!
Hizi ndizo mila zetu
Na utamaduni wetu
Na maadili yetu
Lakini niambie ndugu rafiki ....
Mila na utamaduni wa nani?
Na hayo maadili?
Yanamlinda nani?
Siasa gani hii ...
Inayoyatenganisha Mambo
ya ndani na ya nje Ipate
kuhalalisha ukatili!
By Demere Kitunga
No comments:
Post a Comment